Vyombo

Maelezo kuhusu Vyombo Vyombo Vyombo vya kuhifadhia maji na vinginevyo

Kutumia vyombo vya dhahabu na fedha 1. katika kula na kunywa Ni haramu kuvitumia kwa kauli yake Mtume صلى الله عليه وسلم: (Msinywe kwenye vyombo vya dhahabu na fedha, na msile kwenye sahani zake. Kwani hivyo ni vyao wao ulimwenguni na ni vyetu kesho Akhera) [ Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

Na kwa kauli yake Mtume صلى الله عليه وسلم: (Yule anayekunywa kwenye chombo cha fedha, kwa hakika anaingiza tumboni mwake moto wa Jahanamu) [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

2. Kutumia vyombo vya dhahabu na fedha kwa matumizi yasiyokuwa ya kula na kunywa Inafaa kuvitumia kwa matumizi mengine yasiyokuwa kula na kunywa, kama kutawadhia na mengineo kwa hadithi ilio tangulia kuwa imekaza kuvitumia kwa ajili ya kula na kunywa, na imethubu kwa hadithi ya Ummu Salamah t alikuwa na chombo (juljul) la fedha ambayo ndani yake kulikuwa na baadhi ya nywele za mtume صلى الله عليه وسلم.

Kula kenye chombo cha dhahabu Kula kwenye chombo cha fedha

Kutumia vyombo vilivyolihimiwa kwafedha Inafaa kutumia vyombo vilivyolihimiwa kwa fedha kidogo kuwapo na haja, kwa kuwa imethubutu kwamba kopo la Mtume صلى الله عليه وسلم lilivunjika akapafunga pale palipopasuka kwa silsila ya fedha. [Imepokewa na Bukhari].

Birika ya fedha kwa ajili ya kutawadhia Kutumia chombo kilcholihimiwa kwa fedha

Uvaaji dhahabu kwa wanaume Haifai kwa mwanamume kuvaa dhahabu, kwa hadithi iliyothubutu kutoka kwa Abu Musa al-Ash›ari kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu صلى الله عليه وسلم alisema: (Limeharimishwa vazi la hariri na dhahabu kwa wanaume wa umma wangu na limehalalishwa kwa wanawake wao) [Imepokewa na Tirmidhi].