MAANA YA FURAHA NA HAKIKA ZAKE

MAANA YA FURAHA NA HAKIKA ZAKE Maana ya furaha Neno furaha ni miongoni mwa maneno ambayo watu wametofautiana; kuna miongoni mwao wanaona kuwa ni mwenza wa neno ladha au raha au mali au cheo au umaarufu na kadhalika. Na kwa sababu hiyo watu wengi hupoteza maisha yao katika njia mbali mbali wakitafuta furaha, ndio…furaha ni hisia inayotoka ndani ya nafsi ya mwanadamu anapohisi hali ya kuridhika na utulivu, hata hivyo mtazamo wa watu kuhusu furaha umetofautiana na hii ni kutokana na tofauti tabia zao, mapenzi yao, na matarajio yao, na hata jamii zao, baadhi ya watu wanaiona ipo kwenye mali au makazi au cheo na afya, na wengine wanaiona ipo kwenye mke, au watoto au kazi au masomo na huenda wengine wakaiona ni kuwa ukaribu na mpenzi au katika kuondokana na mtu mwenye kero au katika hisia nzuri ya kiroho au kumsaidia masikini na fukara, ama jambo la kushangaza ni kuwa utakapo wauliza wengi miongoni mwa watu hawa: Je, wewe ni mwenye furaha? Jibu lake litakuwa ni kwa kukataa!!!

Kwa hiyo utaona kuwa taarifu zina tofautiana baina ya mtu na kwa mwingine na jamii moja hadi jamii nyingine, kiasi cha kufanya jumuia ya kimataifa kuweka daraja jina lake daraja la furaha miongoni mwa mataifa, walitaka kujua ni taifa gani lenye furaha zaidi, na hivyo basi kuzipa alama daraja hizi na wakasimamia ufuatiliaji na tafiti mbali mbali, Lakini matokeo yaliwa shangaza wote; hivyo Wamerekani wakawa ndio wenye matatizo zaidi na si furaha, na hawakupata isipokuwa alama za chini kabisa, pamoja na kuwa tunajua hali ya starehe na mas-ala ya anasa kwa watu wake.